KINYUA BIN KING’ORI: Viongozi na raia wahubiri amani uchaguzi mkuu unaponukia

KINYUA BIN KING’ORI: Viongozi na raia wahubiri amani uchaguzi mkuu unaponukia

NA KINYUA BIN KING’ORI

KENYA ni taifa linaloenziwa kote duniani kutokana na historia ya kupalilia umoja na kudumisha amani miongoni mwa wananchi wake licha ya kuwa wa makabila mbalimbali.

Viongozi wetu sasa hawafai kutumia nyadhifa zao walizopewa na umma kuendesha siasa za mivutano na matusi wakati huu wa kipindi cha lala salama za kampeni kuelekea Agosti 9, 2022.

Amani ni wajibu wa kila mmoja wetu kuanzia kwa ‘Wanjiku’ pale kijijini hadi kwa Rais Uhuru Kenyatta akiwa Ikulu ya Nairobi.

Inatia hofu kuona siku za hivi karibuni Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake Dkt William Ruto wakitupiana maneno makali katika mikutano yao.

Viongozi hao wameweka wazi chuki zao kisiasa na huenda wakawa chanzo cha taifa hili kuchukua mkondo mbaya wa chuki na uhasama wa kisiasa kabla na hata baada ya uchaguzi mkuu.

Kwa nini viongozi hao wanalumbana hadharani? Mvutano wao unafaa taifa hili nini wakati huu Wakenya wanalia bei za bidhaa msingi kupanda maradufu?

Katiba yetu imewapa Wakenya uhuru wa kisiasa ambapo kila mtu kwa hiari yake anaweza kushabikia mrengo au kuunga mkono mwaniaji yeyoye wa Urais hadi mwakilishi wadi bila vitisho au kulazimishwa.

Rais na naibu wake wamejipata katika malumbano baada kusalitiana na Rais kuunga mkono hasimu wake Raila odinga wa Azimio huku Dkt Ruto akiwa upande wa Kenya Kwanza.

Mrengo wa Dkt Ruto umekuwa ukilaumu Rais kwa kutumia nguvu serikalini kuwahangaisha wakati wanaendesha kampeni zao.

Viongozi wetu wanafaa kujua mchakato wa uchaguzi mkuu ni wa muda tu na haufai kamwe kuwa chanzo cha kuvuruga au kutishia Umoja na amani.

  • Tags

You can share this post!

Mbogo ajutia uaminifu wake kwa Wiper

Pogba kusakata Kombe la Dunia

T L