Habari Mseto

Kiongozi wa mashtaka ajikanganya katika kesi ya bangi

April 17th, 2020 1 min read

Na Richard Munguti

Kiongozi wa mashtaka Abel Amareba amejipata taabani kuhusu shtaka la mihadarati dhidi ya washukiwa watatu.

“Niko na shida na shtaka dhidi ya Baraza Twaha. Ameshtakiwa aje shtaka la kusafirisha misokoto ya bangi pasi kushtakiwa kwa kupatikana akiwa akiwa na bhangi?” akamuuliza hakimu┬áMartha Nanzushi.

Hakinu huyo alimtaka Amareba afutilie mbali shtaka hilo lakini akafafanua kifungu alichoshtakiwa

Twaha alikanusha shtaka la kusafirisha bangi kinyume cha sheria katika mtaa wa Ngara kaunti ya Nairobi.

Kutoka kulia: Washukiwa wa ulanguzi wa mihandarati Baraza Twaha, Ibrahim Ndolo Wako na Samuel Njabi wakiwa kizimbani. Picha/Richard Munguti

Hakimu alifahamishwa Twaha alitekeleza kosa hilo baada ya kuachiliwa kwa dhamana na mahakama ya Makadara.

Ibrahim na Samuel walikabiliwa na mashtaka ya kupatikana na visu mahali pa umma.

Kila mmoja alishtakiwa kwamba walikuwa wanajiandaa kutekeleza uhalifu mtaani Ngara.