Makala

VIDUBWASHA: Kioo kinachochaji simu (Beauty Bank Compact Mirror)

June 18th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

NI jambo la kawaida kwa akina dada kubeba vioo katika mikoba yao.

Kadhalika, imekuwa kawaida watu kujihami kwa vifaa vya kuhifadhi kawi (powerbank) ili kuhakikisha kuwa simu haziishiwi na chaja.

Kioo cha Compact Mirror kinaondoa usumbufu wa kujaza mkoba kwa vitu vingi kama vile chaja.

Kioo hiki pia ni ‘powerbank’ ya kuchaji simu.

Aidha kina uwezo wa kuhifadhi kawi ya 3000Ah kumaanisha kwamba kinaweza kuchaji simu zaidi ya moja.

Kinaweza kuchaji simu za aina zote kama vile Android au Apple.

Mbali na kuchaji simu, kioo hiki kinaweza kutumiwa usiku gizani kwani kina mwangaza wake.