Kipa Kasper Schmeichel ajiunga na Nice baada ya kuondoka Leicester City

Kipa Kasper Schmeichel ajiunga na Nice baada ya kuondoka Leicester City

Na MASHIRIKA

NAHODHA wa Leicester City, kipa Kasper Schmeichel, 35, ameagana rasmi na kikosi hicho na kuyoyomea Ufaransa kuvalia jezi za Nice.

Schmeichel alichezea Leicester mara 479 tangu asajiliwe kutoka Leeds United. Alisaidia Leicester kuzoa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Kombe la FA na Community Shield. Alikuwa pia sehemu ya kikosi kilichoshindia Leicester Ligi ya Daraja ya Kwanza nchini Uingereza (Championship) mnamo 2013-14.

Anamfuata Aaron Ramsey kambini mwa Nice baada ya kiungo huyo raia wa Wales mwenye umri wa miaka 31 kuondoka kambini mwa Juventus.

Schmeichel anajivunia kuchezea timu ya taifa ya Denmark mara 84.

Leicester ndicho kikosi cha pekee miongoni mwa washiriki wa ligi kuu tano za bara Ulaya ambacho hakijasajili mchezaji yeyote muhula huu. Kocha Brendan Rodgers amekiri kwamba klabu hiyo inapitia hali ngumu ya kifedha.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kibarua kigumu cha Okutoyi robo-fainali ya tenisi ya...

TAMTHILIA: Uongozi mbaya katika Kigogo – 3

T L