Michezo

Kipa Neuer astaafu siku mbili tu baada ya nahodha Gundogan kujiondoa


KIPA Manuel Neuer wa timu ya Ujerumani ametangaza kustaafu kuchezea timu hiyo baada ya miaka 15.

Mlinda lango huyo wa klabu ya Bayern Munich amechezea timu hiyo ya taifa mara 124 tangu 2009.

Mara tu baada ya kutoa uamuzi huo, Shirikisho la Soka Ujerumani (DFB),  lilimtaja mwanasoka huyo kuwa miongoni mwa makipa bora duniani. Neuer alitangaza habari hizo, siku mbili tu baada ya kiungo na nahodha wa timu ya taifa, Ilkay Gundogan, kuamua kustaafu kucheza kimataifa.

Kupitia kwa mtandao wake wa binafsi, kipa huyo mwenye umri wa miaka 38,  aliandika: “Leo ndio mwisho wa kuchezea timu ya taifa. Nimefikiria muda mrefu kabla ya kutoa uamuzi huu.”

Neuer aliyeshinda tuzo ya kipa bora wakati wa Ujerumani Die Manschaft,  aliisaidia Ujerumani kunyakua ubingwa wa Kombe la Dunia mnamo 2014.

Gundogan aliyekuwa nahodha wa timu hiyo wakati wa Euro 2024, amestaafua akiwa na umri wa miaka 33 baada ya kuifungia mabao 19 katika mechi 82. Thomas Muller mwenye umri wa miaka 34 alitangulia kustaafu baada ya kumalizika kwa Euro 2024, timu hiyo ilipoondolewa katika hatua ya robo-fainali.