Kipchoge afungua maktaba kwa umma Kapsisiywa

Kipchoge afungua maktaba kwa umma Kapsisiywa

Na GEOFFREY ANENE
 
MSHIKILIZI wa rekodi ya dunia mbio za kilomita 42 wanaume, Eliud Kipchoge amefungua maktaba katika eneo la Kapsisiywa kaunti ya Nandi, jana Jumatatu.
 
Akitangaza habari hizo, bingwa huyo mara mbili wa Olimpiki, ambaye alisema hapo awali kuwa maktaba hayo yatakuwa ya vitabu vya Sayansi, Teknlojia, Uhandisi na Hisabasti (STEM), alisisitiza elimu ni muhimu kwa maendeleo.
 
“Elimu pia inachangia katika ukuaji na maendeleo katika sekta mbalimbali za maisha. Ninajivunia sana kufungua maktaba ya Eliud Kipchoge ambapo watu kutoka tabaka mbalimbali wanaweza kuja pamoja,” alisema.
 
Katika maktaba hayo, anasema, kila mtu ataweza kupata kujifahamisha kibinafsi na pia kitaaluma. “Yataleta jamii pamoja, kukuza umoja na kushirikiana katika kupeana maarifa. Pamoja tunaweza kuwa na maisha mema ya baadaye!” alisema.
 
Kipchoge, ambaye alipata rekodi ya dunia ya kilomita 42 aliposhinda Berlin Marathon kwa saa 2:01:39 mwaka 2018 nchini Ujerumani, atakuwa akirejea jijini Berlin kwa mbio hizo za haiba mnamo Septemba 25.
  • Tags

You can share this post!

Mahakama ya Juu yatesa wabunge kwa kuzima CDF

Gachagua, Karua wapiga kura Sagana na Mugumo mtawalia

T L