Michezo

KIPENGA: Kumbe Real Madrid walikunywa Alvaro yote na kuuza chupa

April 30th, 2018 2 min read

Na JOB MOKAYA

Msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza unaelekea kukamilika rasmi. Manchester City imetia ligi kibindoni na timu nyingine kubwa zinawania nafasi za 2,3 na 4.

Msimu ulipoanza na pia dirisha fupi la uhamisho lilipofunguliwa, timu kadhaa ziliimarisha vikosi vyao.

Msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza unaelekea kukamilika rasmi. Manchester City imetia ligi kibindoni na timu nyingine kubwa zinawania nafasi za 2,3 na 4.

Msimu ulipoanza na pia dirisha fupi la uhamisho lilipofunguliwa, timu kadhaa ziliimarisha vikosi vyao.

Arsenal ilimsajili Alexandre Lacazette kutoka klabu ya Lyon ya Ufaransa. Lacazette alikuwa nambari mbili katika ufungaji wa mabao katika Ligue 1 msimu uliopita kwa kuona wavu mara 28 katika mechi zote, nyuma ya Edinson Cavani wa PSG aliyefunga mabao 35.

Katika mechi za kujiandaa kwa msimu mpya, Lacazette alionesha kwamba atafanya kweli ndani ya msimu. Alifunga mabao na pia kufanya mashambulizi ya kudhihirisha kwamba atakuwa mchezaji mzuri.

Ingawa huenda asiwe Thiery Henry mpya. Aidha, walinunua Aubumenyang na Henrikh Mkhitariyan kwenye dirisha fupi la uhamisho.

Kwa upande mwingine, Manchester United walinyakua huduma za mchezaji wa zamani wa Everton Romelo Lukaku.

Lukaku alivamia nyavu mara 25 na kuwa wa pili kwa ufungaji nyuma ya Harry Kane wa Tottenham Hotspur aliyezifuma nyavu mara 29 msimu uliopita.

Katika mechi za kujiandaa kwa msimu mpya, Lukaku alionekana kufanya kweli baada ya kufunga mabao kadhaa dhidi ya Manchester City na Real Madrid kwenye mechi ya Super Cup.

Liverpool pia walimnunua mchezaji wa zamani wa Chelsea, Mohamed Salah, raia wa Misri, ambaye pia alionesha makali yake kwa kufunga mabao kadhaa katika mechi za kujiandaa kwa msimu mpya na sasa ndiye mfungaji bora mbali na kuvunja rekodi kadhaa Uingereza.

Swali ni je, mshambulizi mpya wa Chelsea Alvaro Morata atafanikiwa katika timu yake ya Chelsea? La hasha. Aanze kufunganya virago.  Katika mechi za kujiandaa kwa msimu mpya, Morata alionekana kama mtu ambaye hajui mpira. Kama mwanagenzi wa soka.

Kama straika wa kuibukia tu.  Morata hakufunga bao lolote kwenye mechi kadhaa za kujiandaa kwa ligi ambazo Chelsea ilishiriki. Na hali haijawa tofauti ligi ikitamatika. Hafungi mabao mengi.

Hata kocha wake Antonio Conte amepoteza matumaini naye na kuanza kumlisha benchi. Katika mchuano wa Ngao ya Jamii (Community Shield) dhidi ya Arsenal mwanzoni mwa msimu, Morata aliingia katika kipindi cha pili baada ya kumtoa Michy Batshuayi.

Hata hivyo, alionekana kukimbia ovyo uwanjani bila mwelekeo na kutoonekana kama mchezaji wa Pauni milioni 70 (Sh10 bilioni).Hata kwenye mikwaju ya penalti, Morata alipiga penalti mbovu sana na kuwafanya wachezaji wenzake kama Michy kucheka na wengi kushangaa.

Ingawa hata wachezaji nyota hupoteza penalti, namna alivyoipiga yake ilishangaza sana. Mwanzo, mkwaju wake ulikuwa hafifu. Pili, hata haukupanguliwa na kipa. La hasha. Aliupiga nje.

Sioni kama huyu ndiye yule aliyefunga mabao 20 kwa Real Madrid msimu uliopita. Mchezo wake mbovu sasa unafanya wahakiki wengi kujiuliza kama Real Madrid ilikunywa Alvaro yote na kisha kuuzia Chelsea chupa tupu!Alvaro ni aina ya kinywaji kama vile soda.

Naye mchezaji huyu anaitwa Alvaro Morata. Huenda basi Madrid walikunywa Alvaro yote na kuuza Chelsea chupa tupu.