Kipengele 141 cha Katiba: Kuapishwa kwa mshindi wa kiti cha urais

Kipengele 141 cha Katiba: Kuapishwa kwa mshindi wa kiti cha urais

NA SAMMY WAWERU

BAADA ya mgombea atakayetangazwa kuwa mshindi wa urais kufuatia uchaguzi mkuu Agosti 9, 2022, vigezo vya Katiba sharti viheshimiwe na kutekelezwa.

Kipengele cha 141, kimeainisha matakwa hayo ili rais mteule aidhinishwe rasmi kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kiongozi wa nchi.

Kifungu cha kwanza (1), kinaeleza rais mteule ataapishwa machoni mwa umma na Jaji Mkuu (CJ), na endapo CJ hatakuwepo naibu wake (DCJ) amlimshe kiapo.

CJ wa sasa Kenya ni Bi Martha Koome, naibu wake akiwa Philomena Mwilu.

Rais mteule ataapishwa Jumanne ya kwanza, Kifungu cha pili (2) kinaenelezea, siku 14 baada ya matokeo ya urais kutangazwa rasmi na tume ya uchaguzi endapo hakuna atakayeyapinga, kama kinavyosema Kipengele cha 140.

Tayari Mahakama ya Juu imetengeneza kitengo kidogo Milimani, Nairobi ili kujiandaa kupokea kesi yoyote ya kupinga matokeo ya kura za urais za Agosti 9, 2022 endapo itawasilishwa.

“Au, siku ya 7 baada ya makahama kufutilia mbali kesi itakayowasilishwa kortini kupinga atakayeibuka mshindi (ikiwa malalamishi yataibuka),” Katiba inafafanua, Kipengele hicho kikidokeza rais mteule ataanza majukumu yake baada ya kuapishwa.

Bunge la kitaifa, chini ya mamlaka yake, litatoa mwelekeo wa hafla ya uapisho.

Wakati wowote kuanzia sasa Wakenya watatangaziwa rais wa tano wa Jamhuri ya Kenya, na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

  • Tags

You can share this post!

Ruto aingia katika ukumbi wa Bomas

Mshindi wa kiti cha urais Dkt William Ruto atoa hotuba...

T L