Michezo

Kipserem azidi kutamba Rotterdam Marathon

April 7th, 2019 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

NYOTA Marius Kipserem ameendeleza utawala wa Kenya katika mbio za Rotterdam Marathon hadi miaka minne baada ya kuibuka bingwa kwa rekodi mpya ya saa 2:04:11 nchini Uholanzi, Jumapili.

Kipserem, ambaye pia alishinda jijini Rotterdam mwaka 2016, amerejesha taji lake kwa kukamilisha umbali huo wa kilomita 42 kwa muda huo wake bora akifuta rekodi ya Rotterdam Marathon ya saa 2:04:27 ambayo Mkenya Duncan Kibet alitimka mwaka 2009.

Marius Kimutai na Kenneth Kipkemboi walishinda mbio za Rotterdam mwaka 20117 na 2018 mtawalia kabla ya Kipserem kupata taji lake la pili.

Mturuki Kaan Kigen Ozbilen, ambaye ni mzawa wa Kenya, alimaliza katika nafasi ya pili kwa saa naye Mkenya Emmanuel Saina akafunga mduara wa tatu-bora. Taji la wanawake, ambalo Mkenya Visiline Jepkesho alitwaa mwaka 2018, limenyakuliwa na Muethiopia Ashete Bekere kwa saa 2:22:55.

MATOKEO (Aprili 7, 2019):

Wanaume

Marius Kipserem (Kenya) saa 2:04:11

Kaan Ozbilen (Uturuki) 2:05:26

Emanuel Saina (Kenya) 2:05:42

Abdi Nageeye (Uholanzi) 2:06:18

Vincent Rono (Kenya) 2:07:09

Josphat Boit (Kenya) 2:07:20

Wanawake

Ashete Bekere (Ethiopia) saa 2:22:55

Stella Barsosio (Kenya) 2:23:34

Aliphine Tuliamuk (Marekani) 2:26:48

Bethlehem Moges (Ethiopia) 2:27:51

Roberta Groner (Marekani) 2:29:06