Habari Mseto

Kirinyaga yalemewa na corona

August 13th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Watu 35 wamepatikana na virusi vya corona kaunti ya Kirinyaga ambayo bado inajitahidi kufikisha idadi ya vitanda vya kuwatenga wagonjwa wa corona inayohitajika.

Hivi karibuni naibu gavana Peter Ndambiri alisema kwamba kaunti hiyo haiko tayari kupambana na janga la corona.

Alisema kwamba kaunti hiyo ina matatizo ya kifedha kw asababu ya kutoelewana kati ya gavana na madiwani kuhusu bajeti.