Kirui kivutio Fukuoka Marathon Japan, aendea taji la Githae

Kirui kivutio Fukuoka Marathon Japan, aendea taji la Githae

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa dunia mbio za kilomita 42 mwaka 2009 na 2011 Amos Kirui atakuwa kivutio kwenye makala ya 76 ya Fukuoka Marathon nchini Japan hapo Desemba 4.

Kirui, ambaye aliwahi kushinda Chicago Marathon nchini Amerika mwaka 2016 na pia kukamata nafasi ya pili kwenye Olimpiki 2012 mjini London nchini Uingereza, yuko katika orodha ya watimkaji 85 watajika watakaowania taji.

Orodha hiyo ya wakimbiaji watajika pia ina Wakenya Michael Githae, Kenneth Keter, Silas Too, Joel Mwaura, Paul Onyiego, Bethwell Yegon, Amos Kurgat, Donald Mitei na Vincent Raimoi. Githae ni bingwa mtetezi. Too alishinda Eindhoven Marathon nchini Uholanzi mwaka jana.

Onyiego, Yegon, Kurgat na Mitei pamoja na raia wa Australia Jack Rayner watakuwa wawekaji wa kasi.

Rekodi ya Fukuoka Marathon ya saa 2:05:18 inashikiliwa na Muethiopia Tsegaye Kebede tangu ashinde taji la mwaka 2009. Githae alinyakua taji la 2021 akifuatiwa na Mjapani Kyohei Hosoya na Mkenya Rungaru mtawalia. Makala ya 2022 yamevutia jumla watu 12,000. Fukuoka Marathon huwa ya wanaume pekee.

You can share this post!

Ukimwi: Kaunti zalaumu umaskini na dhuluma za kijinsia,...

Waathiriwa wa sumu eneo la Owino Uhuru wapata pigo

T L