Habari Mseto

Kisa cha gari kuchomwa kituoni chachunguzwa

September 1st, 2020 1 min read

Na George Munene

Polisi wanachunguza kisa  kimoja ambapo gari moja lililokuwa limeshikwa na kuwekwa kwenye kituo cha polisi cha Wanguru Kaunti ya Kirinyanga lilichomwa.

Gari hilo aina ya Totota Sienta linalomilikiwa na mwanabiashara mmoja Bw David Murimi lilikuwa limezuliwa kwenye kituo cha polisi baada ya kuhusika kwa ajali ambapo liliua afisa wa polisi. Bw Murimi pia alikuwa kwenye ajali hiyo iliyotokea Aprili barabara ya Embu kuelekea Makutano.

Mfanyabiashara huyo alipingwa na butwaa alipopata gari lake limeteketezwa .

“Baada ya kupona marejaha niliyoyapata kwenye ajali hio nimekuwa nikiomba polisi waachilie gari langu lakini walikataa,”alisema Bw Murithi..

Alikumbuka  jinsi siku hiyo ya Jumamosi polisi mmoja alipompasha habari kwamba gari lake limeteketezwa.

Bw Murimi aliomba kufidiwa gari lake. Alishangaa vipi gari lake linaweza kuteketezwa na watu wasiojulikana na kutoroka kwenye kituo cha polisi ambacho huwa chini ya ulinzi saa zote.

Bw Murimi alisema kwamba alishuku mchezo mchafu na kwamba atapigania ukweli upatikane.

Kamanda wa polisi wa Mwea Madshariki Emmanual Opuru alimwambia mfanyabiashara huyo awe na subira uchunguzi ufanyike. “Tumeanza uchunguzi kutafuta ukweli kuhusu kilichotokea.”

Tafsiri na Faustine Ngila