Dondoo

Kisura afokea mume kudunisha mlo wake


KERONJO, BOMET

JAMAA wa hapa alifokewa na mkewe kwa kudharau upishi wake huku akisifu ubingwa wa mpishi katika hafla walilohudhuria.

Inasemekana polo alikuwa akifurahia wali kwa minofu katika hafla alipofumaniwa na mkewe akimsengenya.

“Nikimletea hata mchele wa bei ghali sana bado ataniandalia wali ulio sawa na sembe! Hakuna haja ya kijiko hata, mtu akiamua atumie mkono kula bado ni sawa tu! Ni kurutu jikoni,” polo akasema asijue mkewe alikuwa karibu.

Azua kisanga ofisini akikabili polo aliyemtumia picha chafu

MOMBASA MJINI

Mwanadada mmoja alizua kisanga katika ofisi moja mjini hapa alipomfokea jombi mfanyakazi mwenzake akimtaka akome kumtumia picha chafu.

Demu alidai jamaa huyo alikuwa na mazoea ya kumtumia picha na video za ponografia licha ya kumuonya mara kadhaa.

Siku ya kisanga, alimkabili jamaa mbele ya wafanyakazi wenzao na kumkanya vikali.

“Ninakuonya mara ya mwisho, ukiendelea kunitumia picha hizo, nitakuchukulia hatua,” demu alifoka kwa hasira na kusema hangemblock jamaa kwa sababu ya mawasiliano ya kikazi.

“Ikiwa hauna chochote cha kuniambia kuhusiana na kazi, usinisumbue na jumbe zako za kishetani,” alisema.

Jamaa aliaibika na wakuu wa kampuni wakamhimiza aombe kipusa msamaha.

Haikujulikana mara moja iwapo jombi alifanya alivyoagizwa.