Makala

VIDUBWASHA: Kitakufaa msimu wa baridi (Nicelucky Coffee Mug Warmer)

March 12th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

KIFAA hiki kinahakikisha kuwa chai au kahawa haipoi inapokuwa kwenye kikombe.

Ukiwa na kifaa hiki cha kidijitali, hakuna haja ya kubeba chupa ya chai kazini au unapojipumzisha nyumbani.

Unachohitaji ni kikombe tu.

Hakitumii betri kwani huunganishwa na stima. Mtumiaji huseti kiwango cha joto analotaka.

Kikombe hiki pia kimetengenezwa kwa muundo wa kuvutia ambao hupamba dawati lako la kazi.

Ni bapa hivyo kikombe hakiwezi kumwaga chai unapokiweka juu yake.

Kinapasha joto aina zote za vikombe hata vilivyotengenezwa kwa plastiki au karatasi ngumu.

Kinatumia kiasi kidogo cha umeme hivyo mtumiaji hapati hasara anapokitumia.

Kinaweza kutumika kupasha kikombe joto kwa siku nzima bila kuonyesha hitilafu.