Kitita cha Sh.6Milioni kilipatikana katika afisi za majaji Muchelule na Chitembwe

Kitita cha Sh.6Milioni kilipatikana katika afisi za majaji Muchelule na Chitembwe

Na RICHARD MUNGUTI

POLISI walipata zaidi ya Sh6.1milioni katika afisi za majaji wawili wa mahakama kuu wanaochunguzwa kwa ufisadi Ijumaa wiki iliyopita.

Katika ushahidi uliowasilishwa kortini jana , Inspekta Felix Karisa Banzi amesema Polisi walipata Dola za Marekani (USD-$)57,000 (sawa na Sh6.1milioni) katika afisi za Majaji Aggrey Muchelule na Said Juma Chitembwe.

Insp Banzi ,ambaye ni mchunguzi kutoka kitengo cha Uchunguzi wa Jinai (DCI) alisema polisi walipata pesa hizo baada ya kupekua afisi hizo.Ushahidi uliowasilishwa na Insp Banzi kupitia afisi ya Mwanasheria Mkuu imebainika Dola za Marekani ($) 50,000 zilipatikana katika afisi ya Jaji Muchelule na Dola za Marekani 7,000 katika afisi ya Jaji Chitembwe.

Kulingana na ushahidi uliowasilishwa katika kesi yao iliyoshtakiwa na chama cha mahakimu na majaji nchini (KMJA) polisi walimpata mwanamke katika afisi ya Jaji Muchelule akiwa na pesa hizo.Ushahidi umesema mwanamke huyo ni broka aliyefikishwa katika afisi ya Jaji Muchelule na Jaji Chitembwe.

Insp Banzi amesema pesa hizo zilichukuliwa na polisi.Ushahidi unasema mwanamke huyo alikuwa amkabidhi Jaji Muchelule pesa hizo.Idara ya DCI imesema majaji hao wanachunguzwa kwa kushiriki ufisadi.Idara hiyo imesema inaendelea kuwachunguza majaji na mahakimu.

Jana Jaji James Makau alisitisha hatua ya kuwafungulia mashtaka majaji hao wawili hadi kesi iliyowasilishwa na KMJA isikizwe na kuamuliwa.Ushahidi huo wa Insp Banzo unatofautiana na ule uliowasilishwa na  Jaji Muchelule kwamba hakuna pesa zozote zilipatikana.

Kesi itasikizwa Oktoba 21, 2021.Majaji Muchelule na Chitembwe wanawakilishwa katika kesi hiyo ya KMJA na mawakili Danstan Omari na Cliff Ombeta.

  • Tags

You can share this post!

Mtihani manaibu 3 wakiendea ugavana

Kaunti yakarabati barabara mbovu ingawa maarufu