Kiungo Danny Drinkwater aomba msamaha kwa ‘kuangusha’ mashabiki wa Chelsea

Kiungo Danny Drinkwater aomba msamaha kwa ‘kuangusha’ mashabiki wa Chelsea

Na MASHIRIKA

KIUNGO Danny Drinkwater atakayebanduka rasmi kambini mwa Chelsea mnamo Juni 2022, amewaomba mashabiki wa kikosi hicho msamaha huku akisisitiza kuwa muda wake ugani Stamford Bridge umekuwa sawa na “mpango wa kibiashara ambao haukuzaa matunda.”

Drinkwater, 32, amechezea timu ya taifa ya Uingereza mara tatu na alisaidia waajiri wake wa zamani wa Leicester City kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2016.

Hata hivyo, nyota yake ilikosa kung’aa kambini mwa Chelsea baada ya kusajiliwa kwa kima cha Sh5.4 bilioni mnamo 2017.

“Nawaomba msamaha mashabiki wa Chelsea. Nimewaangusha pakubwa. Matarajio yenu kwangu yalikuwa mengi ila nimeshindwa kuyafikia,” akasema Drinkwater.

Baada ya makali yake kushuka akiwa ugani Stamford Bridge, Drinkwater alitumwa kwa vipindi vifupi vya mkopo kambini mwa Burnley, Reading, Aston Villa na Kasimpasa ya Ligi Kuu ya Uturuki.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Rift Valley Prisons yalenga kubeba taji la voliboli nchini...

KIKOLEZO: Sema ku-beat!

T L