Michezo

Kiungo Edwin Clifford Omondi ajiunga na Wazito FC

August 19th, 2020 1 min read

Na JOHN ASHIHUNDU

KIUNGO Edwin Clifford Omondi ameagana na Western Stima na kujiunga na Wazito FC.

Kocha Fred Ambani alithibitisha jana kwamba klabu yake imefanikiwa kumpata nyota huyo ambaye pia aliwahi kuchezea Gor Mahia Youth, Palos FC na Chemelil Sugar.

Wazito FC have announced the signing of midfielder Edwin Clifford ‘Euro’ Omondi from Kenyan Premier League club Western Stima.

“Nafurahia kujiunga na Wazito FC kwa sababu ni miongoni mwa timu kubwa nchini Kenya kwa sasa. Lengo langu ni kujiahidi na kuisaidia timu hii kuvuma msimu ujao. Nawaomba mashabiki waendelee kutuunga mkono,” alisema kupitia kwa mtandao rasmi wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL).

Akizungmza kuhusu mchezaji huyo, Ambani alisema anamfahamu kama mchezaji mwenye ujuzi wa kutosha utakaosaidia kikosi chake.

Omindi maarufu kama Euro ni mchezaji wa tano kujiunga na Wazito FC, baada ya ujio wa Vincent Oburu, Mark Otieno, Kevin Kimani na Boniface Omondi.