Kiungo Mkenya ajiunga na klabu ya amputee nchini Uturuki

Kiungo Mkenya ajiunga na klabu ya amputee nchini Uturuki

NA AREGE RUTH

KIUNGO wa timu ya taifa ya Kenya ya Soka ya Amputee Mohammed Munga, amejiunga na klabu yake ya zamani ya Eyyübiye Amputee nchini Uturuki kwa misimu miwili.

Alijiunga na Eyyübiye mnamo 2017 na alimaliza kama mfungaji bora kwa misimu mitatu mfululizo. Msimu wa 2020, alifunga mabao 18 katika mechi tisa alizocheza. Alisaidia timu yake kupanda daraja hadi ligi kuu ya soka ya daraja la kwanza.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Amputee ya kaunti ya Nairobi, ameelezea Taifa Spoti kuwa, alipata mapokezi mazuri na wenyeji wa klabu hiyo.

Wakati huu, wanaendela kunoa makali yao kwa maandalizi ya msimu mpya ambao unaanza hapo kesho Jumamosi.

“Ni nafasi ambayo nimesubiri kwa muda na imefika. Tunajiandaa sasa kwa ligi, Ratiba ya mazoezi ni ya asubuhi na jioni na hii itanisaidia kuingiana vizuri na wachezaji wenzangu,” alisema Munga.

“Mechi yetu ya kwanza tutapiga Jumapili, kutokana na mazoezi haya nina imani tutapata matokeo mazuri. Benchi la ufundi pia limekuwa nasi bega kwa bega kuhakikisha tuna utimamu wa mwili wa kutosha,” aliongezea Munga.

Mchezaji huyo aliwahi kuipigia klabu ya ?anliurfa Eyyübiye nchini Uturuki. Timu hiyo pia ilikuwa nyumbani kwa Mkenya Brian Oroka ambaye kwa sasa yupo nchini. Wakiwa pamoja kwenye timu hiyo, walitwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Amputee ya Uturuki baada ya miaka saba tangu ilipoanzishwa mwaka wa 2014.

  • Tags

You can share this post!

Kenya yahimizwa kuchukua bima dhidi ya majanga

Utata kuhusu mahindi ya GMO wazua maswali tele

T L