Kiungo wa CF Montreal Wanyama hatimaye apata mtoto wa kwanza

Kiungo wa CF Montreal Wanyama hatimaye apata mtoto wa kwanza

Na GEOFFREY ANENE

KIUNGO Mkenya Victor Mugubi Wanyama, 30, na mpenzi wake Serah Ndanu Teshna, 33, wamefichua kuwa wamepata mtoto wao wa kwanza.

Kupitia mitandao ya kijamii, Teshna, ambaye alizaliwa Machi 3 mwaka 1988, amesema, “Tutakuwa malaika wako kila mara hapa duniani. Kukupenda unavyostahili na kukulinda. Kukufundisha na kutembea nawe kila hatua yako.”

Ujumbe huo kutoka kwa mwanahabari huyo uliandamana na picha ya wapenzi hao wakipiga busu pamoja na ya kimalaika huyo ambaye Teshna anasema kuwa amefikisha umri wa siku 40.

Kabla ya kujaliwa mtoto, Serah alikuwa amechapisha picha kadhaa akiwa na ujauzito akitoa shukran zake kwa Mungu kwa safari hiyo nzuri.

Muigizaji huyo wa kipindi cha runinga cha Sumu la Penzi, hajafafanua jinsia ya kimalkia huyo wala jina alilopewa.

Mashabiki wengi wamepongeza nyota huyo wa zamani wa klabu za Celtic, Southampton na Tottenham Hotspur anayechezea miamba wa Canada, CF Montreal.

Hata hivyo, kuna wachache kama B.N Omondi (@jatelaw) na BORN HUMBLE (@oburaoniala) ambao wamemkosoa Big Vic kwa “kutotafuta bibi kutoka jamii yake”.

Wanyama anayetoka kaunti ya Busia anaaminika kupokea Sh1 milioni kila siku nchini Canada (Sh7.2 milioni kila wiki, Sh374 milioni killa mwaka).

Anajenga akademia ya kukuza talanta katika kaunti hiyo na pia analipia karo wanafunzi 19 wanaosoma katika Shule za Upili za Precious Blood, Vihiga Friends High, St Angela’s Girls, Mahiga Girls, Kisumu Girls, St Charles Lwanga High, Asumbi Girls, Buruburu Girls, Sheikh Khalifa Binzayed Al-Nahyan, Agoro Sare, Alliance Girls, St Patricks Iten, Musingu High, Sironga Girls, Nanyuki High, St Joseph Cheptiret, Maranda High, Maranda High na St Brigids Kitale.

You can share this post!

Mawaziri wamng’ang’ania Raila shereheni

Mke asukumia mume mhanyaji kipusa

T L