Kiunjuri ahimili mawimbi ya UDA Mlima Kenya kushinda ubunge

Kiunjuri ahimili mawimbi ya UDA Mlima Kenya kushinda ubunge

NA IRENE MUGO

UCHAGUZI mkuu wa Jumanne ulidhihirisha mkondo mpya Mlima Kenya ambapo viongozi wakongwe waliotawala siasa za eneo hilo walibwagwa.

Ni aliyekuwa Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri pekee ambaye alinusurika, baada ya kutwaa kiti cha eneobunge la Laikipia Mashariki kupitia The Service Party (TSP).

Bw Kiunjuri alimshinda Amin Deddy wa UDA ambaye alikuwa akitetea wadhifa wake.

Bw Kiunjuri alikuwa amehudumu kama mbunge wa eneo hilo kati ya 1997-2017.

Katika Kaunti ya Meru, Gavana Kiraitu Murungi alikuwa akielekea kulemewa na mwaniaji huru Kawira Mwangaza ambaye alikuwa mbunge mwakilishi wa kike kaunti ya Meru.

Wanasiasa wengine ambao walilambishwa sakafu Mlima Kenya licha ya kuwa vigogo kwa miaka mingi ni Jeremiah Kioni (Ndaragwa), Amos Kimunya (Kipipiri), Kanini Kega (Kieni) Moses Kuria na William Kabogo (waliokuwa wakiwania ugavana Kiambu), Gavana wa Laikipia Ndiritu Mureithi na Seneta wa Nyeri Ephraim Maina.

Kushindwa kwa vigogo hao sasa kunapisha sura nyingine za wanasiasa, wengi wakiwika kupitia chama cha UDA anachoongoza Naibu Rais Dkt William Ruto.

  • Tags

You can share this post!

Naibu Mwenyekiti wa ODM Kilifi apoteza kiti cha udiwani

CECIL ODONGO: Sheria ikazwe kuadhibu wanaoeneza matokeo...

T L