Habari Mseto

Kiunjuri azindua chama kipya

June 27th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri amezindua chama chake kipya kujiandaa kwa uchanguzi mkuu wa 2022.

Bw Kiunjuri amezidua chama kwa jina The Service Party huku akisema kitashughulikia masaibu ya wananchi na kuwapa uongozi unaofaa.

“Chama cha TSP kimejotolea kutengeneza njia kwa wanaotaka kuleta mabadiliko kwenye jamii. Tutakuwa sauti ya wananchi na TSP itawaonyesha jinsi ya kuendesha maswala ya siasa zinazohusisha kila mtu,”alisema Bw Kiunjuri.

Chama hicho ambacho ni cha 82 kati ya vyama ambavyo vimesajiliwa humu nchini kufikia sasa kina rangi ya manjano, samawati, nyekundu na nyeupe na umbo la moyo ndani ya mviringo kama nembo.

Waziri huyo wa zamani alisema kwamba hatagombea kiti cha ugavana cha kaunti ya Laikipia mwaka wa 2022. Hii yaweza kufasiriwa kuwa mwanasiasa huyo analenga urais hapo 2022.