Kivumbi chanukia Boston Marathon ikivutia Kamworor, Bekele

Kivumbi chanukia Boston Marathon ikivutia Kamworor, Bekele

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Boston Maraton 2021 Benson Kipruto amekiri atakuwa na presha kutetea taji lake dhidi ya wapinzai wakali akiwemo Muethiopia Kenenisa Bekele mnamo Aprili 18.

Akizungumza baada ya wenyeji wa mbio hizo kutangaza orodha ya wakimbiaji 87 nyota wa kitengo cha wanaume Januari 13, Kipruto alisema, “Kurejea Boston nikiwa bingwa kunasisimua, lakini nahisi kuwa na presha kutetea taji. Hata hivyo, natumai kuwa miongoni mwa mabingwa wa Boston watakaokumbukwa na watu kwa muda mrefu.”

Bekele, ambaye alikosa rekodi ya dunia ya kilomita 42 ya Eliud Kipchoge ya saa 2:01:39 kwa sekunde mbili akishinda Berlin Marathon mwaka 2019, atatimka mjini Boston kwa mara ya kwanza kabisa.

“Najua utamaduni wa Boston Marathon na ninasubiri kwa hamu kutifua vumbi Aprili. Ethiopia imekuwa na historia nzuri Boston na ninataka kuwa miongoni mwa waliofanya vyema hapa,” alisema. Bekele amekuwa akivizia rekodi ya Kipchoge kwa muda na huenda atajaribu tena kuifuta.

Majina mengine makubwa yaliyoorodheshwa kukusanyika katika mji huo nchini Amerika ni bingwa wa zamani wa New York Marathon Geoffrey Kamworor, mshindi wa Milan Marathon Titus Ekiru, na wafalme wa Boston Marathon Lawrence Cherono (2019), Mjapani Yuki Kawauchi (2018) na Waethiopia Lemi Berhanu (2016) na Lelisa Desisa (2015).

Orodha ya baadhi ya washiriki wa Boston:

Kenenisa Bekele, saa 2:01:41 (Berlin, 2019), Ethiopia

Titus Ekiru, 2:02:57 (Milan, 2021), Kenya

Evans Chebet, 2:03:00 (Valencia, 2020), Kenya

Lawrence Cherono, 2:03:04 (Valencia, 2020), Kenya

Bernard Koech, 2:04:09 (Amsterdam, 2021), Kenya

Lemi Berhanu, 2:04:33 (Dubai, 2016), Ethiopia

Lelisa Desisa, 2:04:45 (Dubai, 2013), Ethiopia

Gabriel Geay, 2:04:55 (Milan, 2021), Tanzania

Benson Kipruto, 2:05:13 (Toronto, 2019), Kenya

Geoffrey Kamworor, 2:05:23 (Valencia, 2021), Kenya

Eric Kiptanui, 2:05:47 (Apugnano, 2020), Kenya

Bethwell Yegon, 2:06:14 (Berlin, 2021), Kenya

Geoffrey Kirui, 2:06:27 (Amsterdam, 2016), Kenya

Eyob Faniel, 2:07:19 (Seville, 2020) NR, Italia

Yuki Kawauchi, 2:07:27 (Otsu, 2021), Japan

Albert Korir, 2:08:03 (Ottawa, 2019), Kenya

You can share this post!

Uhuru kuwa kocha mkuu wa ‘Team Raila’

Majagina wapiga tizi kali tayari kuvaana na Uganda

T L