Kivumbi kikali kushushwa kwenye mechi za BNSL

Kivumbi kikali kushushwa kwenye mechi za BNSL

Na JOHN KIMWERE 
KIVUMBI kikali kinanukia wikendi hii kwenye michuano ya kipute cha Betika Supa Ligi ya Taifa (BNSL) muhula huu.
Leo vinara wa ngarambe hiyo, FC Talanta chini ya kocha, Ken Kenyatta itashuka dimbani kukabili Fortune Sacco huku ikilenga kuendeleza mtindo wa kutesa wapinzani wao na kuvuna alama tatu muhimu.
”Niliwahi waambia wachezaji wangu kuwa wawe nyakati zote kuwa makini wanapocheza na wapinzani walio karibu nao,” kocha wa FC Talanta alisema na kuongeza kuwa ushindi wao kwenye mchezo huo utawaongezea tumaini la kufanya kutwaa tiketi ya kufuzu kupandishwa ngazi kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Kwenye ratiba ya migarazano hiyo, Kenya Police inayokamata nafasi ya nne katika jedwali itashuka uwanjani Ruaraka, Nairobi kutifua vumbi dhidi ya Gusii FC. Kocha mpya wa Maafande wa Kenya Police, John Bobby Ogolla anasema anataka wachezaji wake waanze kufanya kweli ili kujiongezea matumaini ya kumaliza kati ya nafasi mbili bora katika jedwali la kipute hicho.
Police itashuka dimbani kushiriki mchezo huo huku ikiumiza majeraha ya kuzabwa bao 1-0 na Kibera Black Stars. Wakati huo huo, wachezaji wawili watakosa kushiriki mechi za wikendi hii baada ya kulambishwa kadi au kadi ya majano.
Mt Kenya United itashuka dimbani kukabili Murang’a Seal bila huduma zake Lameck Omondi aliyelambishwa kadi nyekundu. Naye Peter Abiola wa Soy United amabye ameonyesha kadi ya majano mara kumi kesho atakosekana wakati kikosi hicho kitakapoingia mzigoni kucheza na Migori Youth.
  • Tags

You can share this post!

Makala ya msanii- Davy Dee

Makarios na DN Hotstars zatiga robo fainali Dennis Oliech...