Kivutha akerwa na naibu wake kuegemea kwa Ruto

Kivutha akerwa na naibu wake kuegemea kwa Ruto

Na PIUS MAUNDU

GAVANA wa Makueni Kivutha Kibwana, Jumanne alimshutumu naibu wake, Bi Adelina Mwau kufuatia hatua yake ya kujiunga na mrengo wa Naibu wa Rais William Ruto.

Bi Mwau alikutana na Dkt Ruto jijini Nairobi, Jumanne ambapo alivalishwa kofia ya chama cha United Democratic Alliance (UDA).

“Vuguvugu la ‘Hustler’ linakua kila uchao. Leo asubuhi tulimkaribisha Bi Adelina Mwau, Naibu Gavana wa Makueni, ndani ya UDA. Karibu Mama,” Dkt Ruto aliandika katika mitandao yake ya kijamii.

Lakini Gavana Kibwana, baadaye alifichua kuwa Bi Mwau alikuwa ameahidi kumpelekea Dkt Ruto kundi kubwa la watu lakini wakakataa.

“Ninaweka wazi kwamba watu wa Kaunti ya Makueni wanaunga mkono Azimio la Umoja na hatutabadilisha msimamo huo,” akasema Prof Kibwana.

Bi Mwau alijiunga na UDA siku tatu baada ya Dkt Ruto kukita kambi katika Kaunti ya Makueni ambapo aliandaa mikutano ya kisiasa katika maeneo mbalimbali.Dkt Ruto alishutumu Prof Kibwana kwa kueneza ‘uongo’ kwamba eneo la Ukambani linaunga mkono kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga.

You can share this post!

Mseminari ndani kumiliki filamu za ngono

Sevilla wamsajili Martial kutoka Man-United kwa mkopo

T L