Habari Mseto

Kiwanda kipya cha gesi kujengwa Murang'a

April 5th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Mwekezaji mmoja analenga kujenga kiwanda cha kutengeza mitungi ya gesi katika Kaunti ya Murang’a.

Kampuni hiyo group Excellent Logistics Ltd (ELL), inalenga kuzindua ujenzi wa kiwanda hicho kwa gharama ya Sh1.1 bilioni.

Nchini Kenya, kuna kampuni mbili pekee za kutengeneza mitungi ya gesi, East Africa Spectre na Allied East Africa na ujenzi wa kiwanda hicho kutazifanya kuwa kampuni tatu katika biashara hiyo.

Kulingana na Meneja Mkurugenzi Fred Ngugi, kampuni hiyo inalenga kutwaa nafasi iliyotolewa na serikali katika matumizi ya makaa na kuni.

Tayari pesa za ujenzi wa kiwanda hicho zimetolewa. Pia ELL, itajenga stoo ya kuweka gesi itakayokuwa na uwezo wa kuhimili tani 300 za gesi kwa wakati mmoja.