Habari Mseto

Kizaazaa mochari wanawake wakipigani mwili wa mwanamume

November 18th, 2020 1 min read

BRIAN OJAMAA NA FAUSTINE NGILA

Kulishuhudiwa kizaazaa kwenye chumba cha wafu  hospitali ya Rufaa ya Bungoma wakati wanawake wawili walikuwa wanapiagania mwili wa bwanayao.

Christopher Waswa, mwanamume mzee aliyekuwa na wake wawili na Watoto 16 alifariki baada ya kugonjeka kwa muda mrefu alipokuwa amelazwa hospitalini kwa siku chache.

Mwili wake ulikuwa upelekwe nyumbani kwa mazishi wakati wanawake hao walianza kupigania mwili wa mwanamume huyo.

Bw Waswa  alikuwa fundi wa bao eneo la Mayanja eneo bunge la Bumula alikuwa azikwe nyumbani kwa mke wa kwanza Kabuchai.

Watoto wwa bibi wa pili walitaka babayao azikwe nyumbani wa mamayao.

Bi Anne Nanjala, jamaa ya Mwenda zake aliambia wanahabari kwamba mke wa pili alizua vunjo na faamilia tayari ilikuwa  imekubaliana mahala Bw Waswa atazikwa.

“Mwanamke huyo na wanawe alifika hospitalini wakiwa na gari tofauti wakitaka kuchukua mwili huojambo ambalo lilijua vunjo,”Bi Wanjala alisema kwamba taabu zilianza wkati mke wa pili alificha kitambulisho cha Bw Waswa.

Bi Nanjala alisema kwamba alilazimika kumwoba apeane kitambulisho hicho ili maandalizi ya mazishi yafanyike.

“Nilimwambia kwamba kitambulisho hicho kitarudishwa baada ya kuchukua kibali cha  mazishi na stakabathi ya kifo kupewwa familia,”alisema Bi Nanjala.