Habari

Kizaazaa Nairobi spika Beatrice Elachi akijifungia ofisini

July 28th, 2020 1 min read

Na COLLINS OMULO

KIZAAZAA kimeshuhudiwa Jumanne katika Bunge la Kaunti ya Nairobi ambapo Spika Beatrice Elachi amejifungia ofisini akijaribu kukwepa notisi ya madiwani wanaotaka kumwondoa uongozini.

Madiwani 59 wametia saini notisi hiyo na vilevile wametaka kumkabidhi nakala ya agizo la mahakama la kufutilia mbali uteuzi wa Bw Edward Gichana kama Mhazili – clerk – wa Bunge hilo.

Maafisa wa polisi wamewazuia madiwani hao kuingia ofisini humo.