Habari Mseto

Kizaazaa polisi wakitaka kumkamata Mungatana kortini

August 20th, 2020 1 min read

Na Richard Munguti

Kizaazaa kilizuka katika mahakama ya Kibera Nairobi baada ya juhudi za kumkamata tena mbunge wa zamani w Garsen Danson Muungatana.

“Ona hawa wanataka kunikamata tena,’ Muungatana alimweleza wakili wake Geoffrey Kithi.

Huku akieleza wasi wasi wake, Muungatana alisema “hawa jamaa (akimaanisha polisi) wanataka kunitia pingu.”

Bw Kithi aliwataka maafisa hao watatu wawachane na waziri huyo msaidizi wa zamani.

Mfanyabiashara mshirika wa Muungatana Bw Collins Waweru alitorokea ndani ya mahakama ya Kibera.

Muungatana na wakili wake George Kithi waliondoka nje ya mahakama na kuchukuliwa na gari la teksi