Habari Mseto

Kizimbani kwa jaribio la kuiba hela kwa benki mbili

May 22nd, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

MWENYE duka la kuuza vyakula alishtakiwa Jumatano kwa kughushi hundi za benki mbili.

Livingstone Alwodi Karani alifikishwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Nairobi Bw Francis Andayi na kukanusha kesi tatu dhidi yake.

Bw Karani alikabilishwa na mashtaka ya kujaribu kuibia Bank of India (BoI) zaidi ya Sh2.5 milioni akitumia hundi iliyokuwa imeibwa.

Mshukiwa huyu alikana kuwa hundi aliyokuwa ameiba ilikuwa yake Utkarsh Yashvant Pandit ya Sh2.5 milioni

Muuzaji chakula huyo pia alidaiwa alijaribu kuiba kutoka Prime Bank.

Katika Prime Bank aliwasilisha hundi ya Sh675,000 ya kampuni ya Crown Solutions.

Mahakama ilikataa ombi la mshtakiwa kesi zinazomkabili ziunganishwe zote sizikizwe kama kesi moja.

Mshtakiwa alishtakiwa kwa dhamana. Kesi zitasikizwa Julai 2, 2019.