Habari Mseto

Kizimbani kwa kufanya kazi kwa jengo lisilo na leseni

August 16th, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

VIBARUA 10 walioshikwa Jumatano saa nne asubuhi wakiendelea na kazi walifikishwa kortini kwa kufanya kazi katika jengo lisilo na cheti kaunti ya Nairobi.

Miongoni mwa vibarua hao Charles Mwanthi na Kithusi Sammy walikuwa miongoni mwa wale 10 walioshtakiwa pamoja na mkewe Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu, Bi Susan Wangare Ndung’u na muwekezaji Bw Robert Rukwaro.

Wakili Manases Mwangi aliomba vibarua hao waachiliwe kwa dhamana isiyo ya kiwango cha juu akisema  kuwa “ hawana mapato. Walikuwa wameajiriwa tu kujipatia riziki ya kila siku.”

Bw Mwangi aliomba vibarua hao wapewe nakala za ushahidi.

Kila mmoja aliachiliwa kwa dhamana ya Sh80,000 pesa tasilimu.