Habari Mseto

Kizimbani kwa kuiba pikipiki

March 20th, 2018 1 min read

Stephen Wambura Musa ashtakiwa kwa wizi wa pikipiki yenye thamani ya Sh110,000. Picha/ RICHARD MUNGUTI

Na RICHARD MUNGUTI

MWENDESHAJI pikipiki almaarufu bodaboda alishtakiwa Jumatatu kwa kuiiba kutoka kwa mwajiri wake.

Bw Stephen Wambura Musa, alikana aliiba pikipiki hiyo katika barabara ya Moi jijini Nairobi mnamo Machi 11, 2018.

Musa alidaiwa aliiba Pikipiki hiyo aliyokuwa amepewa na Bw Moroa James Pius.

Kiongozi wa mashtaka Solomon Naulikha alisema mshtakiwa hakurudisha bodaboda hiyo kwa mwenyewe kama walivyokuwa wamekubaliana.

“Naomba uniachilie kwa dhamana,” aliomba mshtakiwa.

“Sipingi mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana,” Bw Naulikha alimweleza hakimu mkuu Ftancis Andayi.

Bw Andayi alimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh50,000 pesa tasilimu