Kimataifa

Kizimbani kwa kumtupia manamke jicho la mapenzi kwa baa

February 25th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAMUME kutoka nchini Scotland amefikishwa mahakamani, akishtakiwa kwa kumfungia mwanamke aliyekuwa akimtaka kimapenzi jicho mara kadha, walipokuwa ndani ya baa.

Bw Grezegorz Kwiecien anatuhumiwa kuwa alimfungia mwanamke huyo jicho mara kadha walipokuwa baa ya Dexy’s iliyoko Jijini Dundee, licha ya hali kiuwa mwanamke huyo alikuwa akikataa tabia yake.

Mwanamume huyo wa miaka 36 aidha anadaiwa kumpata mwanamke huyo na kumtongoza hata baada ya kufukuzwa kutoka baa hiyo kutokana na tabia hiyo.

Mahakama ilielezwa kuwa Bw Kwiecien aidha alijaribu kumbusu mwanamke mwingine jioni hiyo, katika baa hiyo.

Anatarajiwa kufunguliwa mashtaka mnamo Mei 9, baada ya kuachiliwa kwa dhamana, shirika moja la habari kutoka Scotland likaripoti.

Kisa hiki kimetokea wakati idara ya leba huko Scotland kutaka sheria za dhuluma za kingono kubadilishwa, hasa kwa vijana.