Klabu ya Lazio yatozwa faini na rais wake kupigwa marufuku kwa kukiuka masharti ya Covid-19

Klabu ya Lazio yatozwa faini na rais wake kupigwa marufuku kwa kukiuka masharti ya Covid-19

Na MASHIRIKA

KLABU ya Lazio inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia (Serie A), imetozwa faini ya Sh16.8 milioni na rais wake Claudio Lotito kupigwa marufuku ya miezi saba kwa hatia ya kukiuka kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Italia (FIGC), Lazio walikataa kuripoti visa vya kuwepo kwa maambukizi ya corona kambini mwao kuanzia Novemba 2020.

Isitoshe, kikosi hicho kiliruhusu wanasoka watatu kuendelea na mazoezi kambini licha ya vipimo vya afya kubainisha kwamba walikuwa na virusi vya corona.

FIGC pia ilibaini katika uchunguzi wake kuwa Lazio walichezeshwa wanasoka wawili waliokuwa na corona katika mechi mbili za Serie A wakati ambapo walistahili kuwa karantini.

Madaktari wawili wa kikosi cha Lazio pia wamepigwa marufuku ya miezi 12. Kikosi hicho kimefichua azma ya kukata rufaa.

Lazio kwa sasa wanashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la Serie A kwa alama 49, sita nyuma ya mabingwa watetezi Juventus wanaokamata nafasi ya tatu nyuma ya AC Milan (alama 59) na viongozi Inter Milan (alama 65).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kenya yazoa medali 12 ndondi za Afrika Ukanda wa Tatu...

Chelsea yaibuka Klabu Bora ya Mwongo kati ya 2011 na 2020