Michezo

KNH yaanza kuamka dimbani

March 13th, 2019 1 min read

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) ilionyesha dalili za kuzinduka kwenye mechi za Kundi A Ligi ya Taifa Daraja ya Pili baada ya kudhalilisha Magana flowers kwa magoli 6-2 Ugani KNH, Nairobi.

Nayo Thika Allstars ilivunjika rekodi ya Balaji EPZ ya kutoshindwa ilipoilaza mabao 2-0. KNH iliteremka dimbani kwa lengo tu kutesa wageni wao na kuchuna alama zote baada ya kupiga Mwiki United mabao 2-1 wiki iliyopita.

”Sina shaka kupongeza wenzangui kwa kuonyesha mchezo wa kuvutia pia kwa mara ya kwanza mwaka huu kuchuna ushindi mzito,” nahodha wa KNH, Ben Obiri alisema na kuwataka kutembeza mtindo huo kwenye mechi sijazo.

Wachezaji hao walibeba ufanisi huo kupitia Rafaya Limbo aliyepiga kombora mbili safi, nao Soso Aka, Josephat Nyoike, Lawrence Otieno na Victor Makomere kila mmoja alitinga goli moja.

Nacho kikosi cha Jumbo T kilishindwa kushuka Uwanjani Woodley Kibera na kufanya Uweza FC ya kocha, Charles ‘Stam’ Kaindi kutuzwa ushindi wa mezani.

Nazo Mwiki United na Commercial FC zilirejea makwao kwa kicheko baada ya kuzoa bao 1-0 kila moja mbele ya Limuru Olympics na Zetech University mtawalia.