Kocha Alumirah aahidi kuiongoza Harambee Starlets kufuzu fainali za AWCON

Kocha Alumirah aahidi kuiongoza Harambee Starlets kufuzu fainali za AWCON

Na JOHN KIMWERE

KOCHA mpya wa Harambee Starlets, Alex Alumirah amedokeza kuwa atatia bidii kuhakikisha timu hiyo ya kina dada imefuzu kushiriki fainali za Kombe la Afrika (AWCON).

Alumirah amesema hayo baada ya kuzinduliwa na Kamati Huru Inayosimamia Soka Nchini kuwa kocha mpya na kutwaa nafasi ya kocha, Charles Okere. Alumirah atasaidiana na makocha wenzake, Berta Achieng (Thika Queens) na Ann Aluoch (Mathare Women FC).

Katika uzinduzi huo Kamati hiyo ya Jaji Mstaafu Aaron Ringera ilitaja meneja wa kikosi kuwa Martha Karimi.

”Sina budi kupongeza kamati inayosimamia soka nchini kwa kutambua uwezo wangu na kuniteua kuwa kocha kuongoza Harambee Starlets kwenye mechi za kuwania tiketi ya kufuzu kushiriki fainali za AWCON,” kocha huyo alisema na kuongeza kuwa atawajibikia jukumu hilo kadiri ya uwezo wake.

Kibarua cha kwanza kwa kocha kitakuwa kuongoza Harambee Starlets ugenini kukabili wenyeji wao Uganda Crested Cranes Februari 16 kisha kushiriki mchezo wa marudiano hapa nchini Februari 23.

”Ninafahamu kitakuwa kibarua kigumu lakini nina imani tutateua wachezaji watakaofaulu kuzima Uganda,” akasema na kuongeza mara ya mwisho kucheza na Uganda ilikuwa kwenye mechi za Cecafa “na tuliishinda.”

Alidokeza kuwa katika uteuzi wao watawapatia wachezaji wa klabu za KWPL kipau mbele ingawa wapo wasiozidi umri wa miaka 20 watateuliwa kwenye juhudi za kukuza vipaji vyao na kuwaanda kutwaa nafasi za wenzao wakistaafu.

Kenya ilifuzu kushiriki mechi za raundi ya pili baada ya kung’ata Sudan Kusini kwa jumla ya mabao 15-0 kati ya mikondo miwili iliyoandaliwa jijini Nairobi kwa sababu za kiusalama nchini mwao.

Alumirah ni kocha mzoefu ambaye hufunza klabu ya Tiger Queens nchini Tanzania anayejivunia mengi katika mchezo huo.

Kocha huyo anajivunia kuongoza Vihiga Queens kutwaa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake nchini Kenya  (KWPL) mara tatu mfululizo.

 

  • Tags

You can share this post!

Borrusia FC yajitoma katika nusu-fainali za Koth Biro

‘Kenya ingali inakabiliwa na changamoto za kuwapata...

T L