Kocha Duncan Ferguson aagana na Everton ili ajikuze zaidi kitaaluma

Kocha Duncan Ferguson aagana na Everton ili ajikuze zaidi kitaaluma

Na MASHIRIKA

KOCHA msaidizi wa Everton, Duncan Ferguson, ameagana rasmi na kikosi hicho kwa matumiani ya kuwa mkufunzi kamili kadri anavyolenga kujikuza zaidi kitaaluma.

Ferguson, 50, anajivunia kufanya kazi na makocha mbalimbali ugani Goodison Park na amewahi kushikilia mikoba ya Everton mara mbili – mnamo Disemba 2019 na Januari 2022.

Ferguson alifungia Everton mabao 73 kutokana na mechi 273 katika awamu mbili tofauti kati ya mwaka wa 1994 na 2006.

“Maamuzi ya kuondoka Everton yamekuwa magumu. Hata hivyo, imebidi niondoke ili nielekee kwingine. Kuwa kocha mshikilizi na naibu wa kocha mkuu kambini mwa Everton kumeniaminisha zaidi katika safari hii ya ukufunzi,” akasema Ferguson.

Ferguson alishikilia mikoba ya Everton kwa kipindi kifupi baada ya Marco Silva kutimuliwa na kabla ya Carlo Ancelotti kuajiriwa, kisha Rafael Benitez alipofurushwa na nafasi yake kujazwa Frank Lampard.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Serikali yaibuka na mikakati ya kushusha gharama ya chakula...

Christian Eriksen akubali kujiunga na Man-United baada ya...

T L