Kocha Marcelo Bielsa arefusha muda wa kuhudumu kwake Leeds United

Kocha Marcelo Bielsa arefusha muda wa kuhudumu kwake Leeds United

Na MASHIRIKA

KOCHA Marcelo Bielsa ametia saini mkataba mpya wa mwaka mmoja kambini mwa Leeds United ambao watakutana na Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Agosti 14, 2021 ugani Old Trafford.

Mkataba wa awali kati ya Leeds United na mkufunzi huyo raia wa Argentina ulitamatika rasmi mnamo Juni 30, 2021.

Bielsa, 66, alijiunga na Leeds United mnamo 2018 na akaongoza kikosi hicho kurejea katika EPL mnamo 2020 baada ya kukaa nje kwa kipindi cha miaka 16.

Mabingwa hao wa Ligi ya Daraja ya Kwanza (Championship) mnamo 2019-20 walikamilisha kampeni za EPL mnamo 2020-21 katika nafasi ya tisa.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Pigo kwa Arsenal baada ya Sheffield United kumkwamilia kipa...

Phil Foden kukosa mechi tatu za kwanza za Manchester City...