Kocha Southgate aogopa kikosi cha Senegal

Kocha Southgate aogopa kikosi cha Senegal

NA JOHN ASHIHUNDU

MECHI mbili za kuwania nafasi ya kufuzu kwa robo-fainali zinapigwa kesho Jumapili, lakini inayozungumziwa zaidi duniani ni kati ya Uingereza na mabingwa wa Afrika, Senegal ambayo itaanza saa nne usiku, ugani Al Bayt Stadium.

Akizungumza kuhusu mechi hiyo, kocha wa Uingereza Gareth Southgate alisema, kulingana na msimamo wa viwango vya Kimataifa vya FIFA, kikosi chake kinaorodheshwa miongoni mwa tano bora.

Lakini nyota huyo wa zamani wa Chelsea ameonya kwamba Senegal inayokamata nafasi ya 18 imeonyesha kiwango kizuri katika mechi za kufuzu.

“Senegal ina wachezaji kadhaa wanaochezea klabu za ligi kubwa barani Ulaya, ikiwemo Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Alisema mabingwa hao wa Afrika wana jina kubwa la kuhifadhi, baada ya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu kwa raundi hii. Itakumbukwa kwamba waliwahi kutinga hatua ya robo-fainali mnamo 2002, na baadaye  kubanduliwa katika hatua ya makundi mnamo 2018.

Kocha Aliou Cisse ambaye ni nyota wa zamani aliyecheza na mastaa wastaafu kama Tony Sylvia, Lamine Diatta na El Hadji Diouf amesisitiza kwamba hawana mpango wa kutwaa ubingwa, lakini wanataka kuwacha historia ya kukumbukwa milele.

“Tuko tayari kukabili Uingereza kesho Jumapili na tnachotaka ni kutengeneza heshima ya kukumbukwa milele. Tunataka kuonyesha ulimwengu kwamba tuko tayari kabisa kwa upinzani wowote.”

Ushindi wao wa kufuzu kwa hatua ya maondoano Jumanne baada ya kuibwaga Ecuador 2-1 ulishangiliwa kwa muda mrefu baada ya mechi kumalizika.

Senegal wanacheza bila mshambuliaji tegemeo, Sadio Mane aliyeumia nchini Ujerumani akichezea Bayern Munich, siku chache kabla ya kuanza kwa fainali hizi.

Miongoni mwa wachezaji wanaosakatia timu kubwa barani Ulaya ni Kalidou Koulibaly na Edouardo Mendy wanaochezea Chelsea, Ismailia Sarr wa Watford pamoja na Idrissa Gueye wa Everton.

Katika kikosi chake cha wachezaji 25, Cisse anajivunia huduma za washambuliaji wanaotamba zaidi kwenye ligi mbalimbali msimu huu.

Awali kwenye mechi nyingine itakayochezewa Al-Thumama, mabingwa watetezi Ufaransa chini ya kocha Didier Deschamps watakabiliana na Poland. Maarufu kama Les Bleus, Ufaransa ilimaliza katika nafasi ya kwanza katika Kundi D, wakati Poland wakimaliza katika nafasi ya pili katika Kundi C.

  • Tags

You can share this post!

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Korea Kusini sasa kutoana jasho...

Kiungo Wyvonne Isuza astaafu soka

T L