Kocha wa Kangemi Allstars asema heri kuvuna alama moja kuliko kupoteza

Kocha wa Kangemi Allstars asema heri kuvuna alama moja kuliko kupoteza

NA PATRICK KILAVUKA

KOCHA wa Kangemi Allstars Paul Okatwa amesikitika kwamba timu yake ilipoteza nafasi nyingi sana ambazo zingeipa ushindi katika mchuano wa Ligi ya Kitaifa Daraja la Kwanza dhidi ya Buruburu Sports uwanjani Kihumbuini, Jumapili.

Hata hivyo, alisema afadhali kuvuna alama kuliko kuambulia patupu. Mechi iliisha sare tasa.

Aidha, kocha wa Buruburu Sports Patrick Orwako alikiri kwamba, walitumia mbinu ya kulinda lango kuwadhibiti Allstars kwa sababu wanawajua kutumia mbinu ya ufumaji wa mbali kuvuruga wapinzani hali ambayo iliwarudisha mchezoni katika kipindi cha pili.

Kangemi Allstars (jezi nyeupe) ikicheza dhidi ya Buruburu Sports (jezi nyekundu) uwanjani Kihumbuini. PICHA | PATRICK KILAVUKA

Kwingineko, Real Stars walivuna alama tatu muhimu baada ya kuwararua UoN Red City 1-0 katika mchuano wa Ligi ya FKF, Kaunti -Ndogo, Nairobi West ambao uliandaliwa uga uo huo. Bao hilo la pekee ambalo lilizamisha chombo za City lilipachikwa kimiani kupitia Dominic Kibet kunako dakika ya 64.

Kwenye patashika ya Ligi ya Kaunti ya Shirikisho la Soka Nchini, Nairobi West, Pelico Jam ilizaba FC Talents 1-0 kupita bao la Hamisi Shaban kunako dakika ya 23.

Pelico Jam (jezi kijani kibichi) ikicheza dhidi ya FC Talents (jezi nyeusi) uwanjani Kihumbuini. PICHA | PATRICK KILAVUKA
  • Tags

You can share this post!

Hakimu amkemea Rigathi Gachagua

Baadhi ya wakazi wa Thika washerehekea baada ya Karua...

T L