Kocha wa kike alivyokwea kuwa mkali wa karate

Kocha wa kike alivyokwea kuwa mkali wa karate

Na LAWRENCE ONGARO

ELIZABETH Rukwaro ni mwanadada ambaye maisha yake karibu yote amezamia katika mchezo wa karate.

Alianza kurusha mateke ya karate akiwa mchanga wa miaka 10 baada ya kupata motisha kutoka kwa nduguye mkubwa Francis Rukwaro, aliyekuwa mwanakarate.

Baadaye miaka za 90 na 2000, mwanadada huyo alihamia kaunti ya Siaya kutoka Nyahururu ambapo alikita kambi na kujiunga na timu ya Siaya Tigers karate club.

Rukwaro 50 ambaye anakamata mshipi mweusi wa 5 th Dan, amewahi kuchezea timu ya Kitaifa kwa zaidi ya miaka kumi huku akisafiri nchi kadha za bara Afrika na ulaya.

Baadhi ya nchi za Afrika amezuru ni Afrika Kusini, Algeria, Rwanda na Tanzania. Pia amesafiri Uingereza.

Ameshindwa medali ya dhahabu kwa mchezo wa kumite kule Uingereza na mchezo wa Kata akazoa fedha kwa mashindano ya kimataifa.

Anatoa wito kwa serikali kuinua mchezo wa karate kwa sababu vijana wengi wamezamia katika mchezo huo.

Baada ya kustaafu kutoka kwa mchezo wa karate mwaka wa 2012, alijitolea mhanga kuona ya kwamba anawajali vijana wanaodhulumiwa mitaa

Akiwa mjini Thika alisononeka sana aliposhuhudia vijana wadogo hasa wasichana katika kitongoji duni cha Kiandutu wakidhulumiwa, kimapenzi.

Mwaka wa 2008 aliamua kuunda klabu cha vijana chipukizi ya Young Dragon karate Club.

Kaunti ya Kiambu na wahisani ndio ambao walitoa ufadhili wa kifedha na kununua vifaa vya michezo.

Lengo lake kuu ni kuwapa mafunzo kamili ya karate ili nao wawe na ujuzi wa kujikinga kutoka kwa maadui wao.

Kocha huyo ambaye ndiye mwanakarate wa kipekee wa kike Thika na kaunti ya Kiambu, tayari amebadilisha maisha ya vijana wengi.

Vijana waliopitia mikononi mwake wamebadilisha maisha yao Kwa kuwa na nidhamu

Wengi wa vijana hao wanatoka kijiji cha kiandutu, ngamia, na kiang’ombe zote ziko vitongoji duni mjini Thika.

Kwa wakati huu mkufunzi huyo anajivunia kuwa na vijana chipukizi wapatao 65 ambao wengi wao ni wanakarate wa kike na wavulana wachache.

Wazazi wengi kutoka vijiji hivyo wamepongeza juhudi za kocha huyo ya kuwanoa vijana hao kuwa na maadili mazuri katika jamii.

Kocha huyo pia asema chipukizi hao wameweza kusafiri hadi nchi za nje kwa kushiriki mashindano ya kimataifa.

Baadhi ya nchi walizozuru ni India, Uingereza, na uhispania kwa michezo ya kimataifa na kuzoa medali kadha.

Vijana wengi waliopitia mikononi mwa kocha Rukwaro ni vijana stadi ambao wanaweza kujikinga vyema kutoka kwa adui yeyote yule.

Mkufunzi huyo asema yeye kama mwanadada angetaka kuacha kumbukumbu katika mchezo wa karate kutokana na mchango wake kwa vijana chipukizi.

Vijana wengi waliopitia mikononi mwa gwiji huyo wa karate wamekuwa kielelezo katika jamii kutokana na kuonyesha nidhamu na kuwa watiifu kwa jamii.

Matarajio ya kocha huyo kwa siku za usoni ni kuona ya kwamba klabu chake kimepiga hatua na kuwakuza vijana chipukizi kuendeleza mchezo huo.

Kocha huyo anawaomba wahisani popote walipo hasa kaunti ya Kiambu kujitokeza kuona ya kwamba inawainua wanakarate chipukizi.

  • Tags

You can share this post!

Winga anayewinda nyayo za Lionel Messi kisoka

Msikubali kutishwa na UDA, Uhuru aambia polisi

T L