Michezo

KOMBE LA DUNIA: Eriksen aondoka kambini kusherehekea mtoto wa kwanza

June 7th, 2018 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

CHRISTIAN Eriksen amekimbia nyumbani nchini Denmark kujiandaa kusherehekea kupata mtoto wake wa kwanza.

Vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti kwamba kiungo huyu wa Tottenham Hotspur ameruhusiwa kutoka kambi ya mazoezi ya Kombe la Dunia kujiunga na mkewe Sabrina Kvist Jensen.

Eriksen, 26, ndiye tegemeo la Denmark katika kindumbwendumbwe hiki kitakachofanyika Juni 14 hadi Julai 15 nchini Urusi.

Itakumbukwa kwamba Eriksen alichangia mabao matatu yaliyosaidia Denmark kunyamazisha Ireland 5-1 katika mechi ya marudiano ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2017.

Kocha Age Hareide alikubali nyota huyu wake kusafiri hadi nyumbani, lakini anatumai hatuchukua muda mwingi mjini Middelfart, huku mechi ya Denmark ya ufunguzi ya Kundi C ikinukia dhidi ya Ufaransa hapo Juni 26.

Eriksen alikuwa na msimu mzuri sana 2017-2018 na Spurs alipoifungia mabao 14 katika mashindano yote na kuisaidia kumaliza Ligi Kuu ya Uingereza katika nafasi ya tatu. Pia alimega pasi 10 zilizozalisha mabao.