KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Ghana walima Korea Kusini na kuweka hai matumaini ya kuingia 16-bora

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Ghana walima Korea Kusini na kuweka hai matumaini ya kuingia 16-bora

Na MASHIRIKA

GHANA walidumisha matumaini ya kutinga raundi ya 16-bora kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea Qatar baada ya kupepeta Korea Kusini 3-2 katika pambano lao la Kundi H uwanjani Education City mnamo Novemba 29, 2022.

Mabingwa hao mara nne wa Kombe la Afrika (AFCON), walifunga kipindi cha pili wakijivunia uongozi wa 2-0 baada ya kuwekwa kifua mbele na Mohammed Salisu na Mohammed Kudus.

Hata hivyo, utepetevu mwanzoni mwa kipindi cha pili nusura uwaponze vijana hao wa kocha Otto Addo baada ya Korea Kusini kufungiwa magoli mawili ya haraka na Cho Gue-Sung. Kudus alifungia Ghana bao la tatu na la ushindi kunako dakika ya 68.

Matokeo ya Ghana yanatarajiwa sasa kuwapa motisha zaidi kadri wanavyojiandaa kufunga kampeni za makundi dhidi ya Uruguay mnamo Disemba 2, 2022 ugani Al Janoub. Korea Kusini watavaana na Ureno katika mechi yao ijayo uwanjani Education City.

Ghana walianza kampeni zao nchini Qatar kwa kichapo cha 3-2 kutoka kwa Ureno uwanjani 974 huku Korea Kusini wakilazimishia Uruguay sare tasa mjini Al Rayyan.

Mechi ya Novemba 28, 2022 ilikuwa ya 10 kati ya Korea Kusini na Ghana ambao sasa wamefunga bao katika kila mojawapo ya mapambano sita yaliyopita ya Kombe la Dunia.

Kufikia sasa, Ghana wanakamata nafasi ya pili katika Kundi H kwa alama tatu, tatu nyuma Ureno wanaoselelea kileleni baada ya kutandika Ureno 2-0 mnamo Jumatatu usiku ugani Lusail Iconic. Uruguay waliodengua Ghana kwenye robo-fainali za Kombe la Dunia mnamo 2010 nchini Afrika Kusini, wanavuta mkia kwa alama moja sawa na Korea Kusini.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Korti yazima serikali kuagiza mahindi tata

Viongozi washinikiza Kuria atimuliwe kwa mpango wake wa GMO

T L