KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Uhispania wabebesha Costa Rica gunia la mabao katika mechi ya Kundi E

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Uhispania wabebesha Costa Rica gunia la mabao katika mechi ya Kundi E

Na CHRIS ADUNGO

CHIPUKIZI Pablo Gavi, 18, alidhihirisha ukubwa wa uwezo wake uwanjani kwa kufunga bao na kuchochea Uhispania kuponda Costa Rica 7-0 katika mchuano wa Kundi E kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar.

Ferran Torres alipachika wavuni mabao mawili katika pambano hilo lililotamalakiwa na Uhispania – mabingwa wa Kombe la Dunia 2010 – kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Gavi ndiye mwanasoka mchanga zaidi kuwahi kuchezea Uhispania katika Kombe la Dunia na bao lake dhidi ya Costa Rica lilimfanya kuwa mchezaji wa umri mdogo zaidi baada ya Pele wa Brazil mnamo 1958 kuwahi kufunga bao katika fainali za Kombe la Dunia.

Ushindi wa Uhispania unatarajiwa kuwatia motisha zaidi kadri wanavyolenga sasa kumenyana na Ujerumani waliokomolewa na Japan 2-1 katika mechi nyingine ya Kundi E.

Uhispania waliotinga nusu-fainali za Euro 2020, walianza mechi kwa matao ya juu na wangalifunga mabao mawili chini ya dakika 10 ila Dani Olmo na Marco Asensio wakapoteza nafasi za wazi walizozipata.

Ulikuwa mwanzo mbaya kwa Costa Rica waliotinga robo-fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Kikosi hicho ndicho kilikuwa cha mwisho kufuzu kwa fainali za Qatar mwaka huu.

Hadi waliposhuka dimbani dhidi ya Costa Rica, Uhispania walikuwa wamepoteza michuano ya ufunguzi kwenye makala matatu ya awali ya fainali za Kombe la Dunia, ikiwemo mwaka wa 2010 ambapo walijinyanyua upesi na kutwaa ufalme nchini Afrika Kusini.

Ujerumani wataaga fainali za Kombe la Dunia mwaka huu iwapo wataangushwa na Uhispania mnamo Novemba 27, 2022 ugani Al Bayt.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Ruto azingatie ahadi yake ya kutoangusha...

KINYUA KING’ORI: Serikali itathmini upya mpango wake...

T L