Michezo

Kombe la UEFA ni la Barca, Ole Gunnar asema baada ya kichapo

April 18th, 2019 1 min read

JOHN ASHIHUNDU

MANCHESTER, Uingereza

Baada ya kushuhudia Barcelona wakisakata soka ya hali ya juu ugani Camp Nou, Jumatano usiku kocha wa Ole Gunnar Solskajer wa Manchester United amesema klabu hiyo ya La Liga ndiyo itakayotwaa ubingwa wa msimu huu.

Ole Gunnar aliwaambia waandishi kwamba kiwango cha vijana hao wa kocha Velvarde kipo zaidi kuliko timu nyingine kwa sasa.

Barcelona iliicharaza United mabao 3-0 kuongezea kwa kijapo kingine cha awali cha 1-0 cah mkondo wa kwanza.

“Nionavyo, Barcelona, wakiwa na safu hiyo ya ushambuliaji, hata wakiamua kuanzisha Dembele na Malcom, watababaisha timu yoyote kwa sasa na sioni taji la msimu huu wakikosa,” alisema baada ya mechi hiyo ya robo-fainali.

“Tulianza vizuri, lakini baada ya muda kusonga tukaanza kuchanganyikiwa kwa sababu tulikuwa tukicheza dhiudi ya timu bora duniani,” aliongeza.

Barcelona wamekuwa wakikosa kupita hatua ya nusu fainali kwa misimu mitatu iliyopita na bila shaka watajitahidi Zaidi wakati huu.