Koo 7 zasaka maafikiano kabla uchaguzi

Koo 7 zasaka maafikiano kabla uchaguzi

Na GEORGE SAYAGIE

VIONGOZI kutoka koo saba za jamii ya Wamaasai Kaunti ya Narok, wameanza mazungumzo kwa lengo la kushirikiana kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Kulingana na viongozi hao wakiwemo wataalamu na Baraza la Wazee kutoka maeneo bunge yote sita ya kaunti hiyo, watakutana ili kutia motisha jamii yao, kufanya uamuzi wa pamoja kwenye uchaguzi na kuimarisha nafasi yao kisiasa na kimamlaka.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la amani la Kaunti ya Narok, Bw Selela Ole Mwanik, Mzee Kelena Ole Nchoe ( mwenyekiti wa baraza la wazee), viongozi hao walifanya mkutano katika boma la mwanasiasa wa eneo la Narok Kusini, Tikoishi Ole Nampaso na kukubaliana kuwa kuna haja ya kuzika tofauti za kiukoo kwa manufaa ya jamii na kaunti yao.

“Tumefanya mikutano sita kabla ya huu lakini leo tumeamua kushirikisha wanahabari waangazie ajenda yetu ya kuunganisha koo zote Kaunti ya Narok,” alisema Bw Mwanik.

Katika chaguzi zilizopita, siasa za koo na kikabila ziliamua mshindi wa viti katika kaunti iliyo na koo za Purko, Loita, Moitanik, Keekonyokie, Ildamat, Siria na Uasin Gishu.

Kuna pia jamii ya Kipsigis katika kaunti hiyo.

Bw Mwanik alisema kwamba ajenda yao pia inatekelezwa na jamii za Maa kaunti za Kajiado, Samburu, Laikipia na Baringo.

You can share this post!

Tahadhari mafuriko yakiua 3 Makueni

MOHAMED OSMAN: Mapendekezo ya Glagsow kuhusu mabadiliko ya...

T L