Koome atofautiana na Maraga

Koome atofautiana na Maraga

Na WINNIE A ONYANDO

JAJI Mkuu mteule Martha Koome ametofautiana na mtangulizi wake, David Maraga kuhusu pendekezo la kutaka kubuniwa kwa afisi ya kupokea malalamishi dhidi ya maafisa wa mahakama (Ombudsman).

Jaji Koome aliyekuwa akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge kuhusu Haki na Masuala ya Sheria (JLAC) iliyokuwa ikimpiga msasa, alisema hana pingamizi zozote dhidi ya afisi hiyo ambayo imependekezwa katika Mswada wa Mpango wa Maridhiano (BBI).

“Naunga mkono kubuniwa kwa afisi hiyo kwani itahakikisha idara ya mahakama inawajibika na kufanya kazi ipasavyo,” akasema Jaji Koome.

Pendekezo hilo lilipingwa vikali na mtangulizi wake Maraga aliyeshikilia kuwa afisi hiyo itasababisha mgongano wa majukumu na Tume ya Huduma ya Mahakama (JSC).

Jaji mkuu mstaafu Maraga alisema majukumu yanayopendekezwa kufanywa na afisi hiyo tayari yanatekelezwa na JSC. “Kuwepo kwa afisi hiyo ni kupokea malalamishi kutaleta amani na umoja kati ya mahakama, bunge na serikali kuu” akasema Koome.

 

You can share this post!

Ajabu ya shule moja kuandikisha ‘E’ kwenye masomo yote...

Aguero kuyoyomea Barcelona mwishoni mwa msimu