Korir kutetea taji la New York Marathon mnamo Novemba 6

Korir kutetea taji la New York Marathon mnamo Novemba 6

Na GEOFFREY ANENE
 
MKENYA Albert Korir atatetea taji lake la mbio za New York Marathon nchini Amerika mnamo Novemba 6.
 
Waandalizi wa mbio hizo za kifahari za Marathon Kuu Duniani (WMM) wametangaza orodha ya washiriki wakisema Korir, ambaye alitawala pia marathon za Houston, Ottawa na Vienna, atakabiliana na nambari mbili jijini New York mwaka 2021 Mohamed El Aaraby kutoka Morocco na bingwa wa London Marathon 2020 Shura Kitata kutoka Ethiopia.
 
Pia, kuna bingwa wa Boston Marathon Evans Chebet ambaye ni Mkenya. Chebet, ambaye amemaliza Berlin, London na Tokyo marathon ndani ya tano-bora, atakuwa akishiriki New York Marathon kwa mara ya kwanza kabisa.
 
Washiriki wengine wa kitengo hicho cha wanaume watakaokusanyika New York mwezi Novemba ni Mbrazil Daniel Do Nascimento, Mjapani Suguru Osako, Mholanzi Abdi Nageeye na Mwamerika na bingwa wa Chicago Marathon 2017 Galen Rupp.
 
“Nafurahia sana kuwa narejea New York baada ya ushindi wangu mwaka jana, lakini pia nahisi kitakuwa kibarua kutetea taji. Nafanya mazoezi makali ili niwe mmoja wa watu wachache sana wamefaulu kuhifadhi taji,” alisema Korir.
 
Waamerika wengine watakaokuwa katika laini ya kuanza mbio ni Abdi Abdirahman, Shadrack Kipchirchir, Elkanah Kibet, Scott Fauble, Ben True, Jared Ward na Leonard Korir.
  • Tags

You can share this post!

Wakongwe kwa vijana wajitokeza kupiga kura Kwale

Wachache wajitokeza kupiga kura Thika na Ruiru

T L