Korti ya Juu yakataa barua ya mpigakura

Korti ya Juu yakataa barua ya mpigakura

NA RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA ya Juu mnamo Ijumaa ilimshauri mpigakura aliyewasilisha barua akiomba matokeo ya uchaguzi wa rais yabatilishwe awasilishe kesi badala ya kuandika barua.

Bw Alfred Juma Ayori aliomba korti hiyo ibatilishe uchaguzi wa Rais Mteule Dkt William Ruto na kufutilia mbali zoezi la kuapishwa kwake na naibu wake Rigathi Gachagua.

Katika barua iliyoandikiwa Jaji Mkuu Martha Koome, alipinga kuapishwa kwa Dkt Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua akisema zoezi la kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9,2022 lilikumbwa na ufisadi.

Lakini idara ya Mahakama ilimshauri Bw Ayora awasilishe kesi ya kupinga uchaguzi wa Ruto na Gachagua.

Uchaguzi wa Urais unaweza kubatilishwa tu endapo kesi itawasilishwa katika Mahakama ya Juu kwa mujibu wa sheria.

Bw Ayora alielezwa apate ushauri wa wakili apate mwongozo ufaao.

Hata hivyo barua hiyo ilipokewa na afisi ya Jaji Mkuu na kupigwa muhuri.

Katika barua hiyo Bw Ayiro alisema ni haki yake kuhoji utaratibu wa kuendeleza zoezi la uchaguzi kwa vile sheria inaitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka kuendeleza uchaguzi kwa njia iliyo huru na haki.

  • Tags

You can share this post!

Uhuru ashikilia ufunguzi wa Bunge la Kitaifa

TUSIJE TUKASAHAU: Uvutaji sigara una madhara

T L