Korti yaamua kesi ya kuzuia Sonko iendelee hadi mwisho

Korti yaamua kesi ya kuzuia Sonko iendelee hadi mwisho

NA PHILIP MUYANGA

MAHAKAMA Kuu imekataa ombi la kutupwa kwa kesi inayotaka aliyekuwa gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, azuiwe kuwania ugavana Mombasa.

Huku akimkubalia mmoja wa waliowasilisha kesi hiyo Mombasa ajiondoe, Jaji John Mativo wa Mahakama Kuu ya Mombasa alisema kesi hiyo itaendelea hadi mwisho.

Mlalamishi, Bw Ndoro Kayuga, alikuwa ameambia mahakama alitambua kuwa kesi haikuwa na uzito ndiposa akaomba kujiondoa wiki chache zilizopita.

Jaji Mativo alisema kujiondoa kwa mlalamishi huyo hakutaathiri kivyovyote kesi iliyowasilishwa.

Kulingana na jaji, mlalamishi wa pili, Bw George Odhiambo, ataendelea kuwakilisha malalamishi yaliyopelekwa mahakamani.

Katika uamuzi wake, masuala yaliyotajwa na Bw Kayuga alipoomba kujiondoa hayakutosha kushawishi mahakama isitishe kesi nzima.

Kulingana na mahakama, kesi inaweza tu kusitishwa kama maslahi ya umma hayataathirika, kama hakuna utumiaji mbaya wa mfumo wa sheria, na kama washirika wanachukua hatua kwa nia njema.

Jaji alisema maamuzi yote hayo yanayotolewa yanazingatia sheria na usawa.

Bw Odhiambo, kupitia kwa wakili wake, Bw Willis Oluga, alikuwa amepinga ombi la Bw Kayuga akisema angependa kesi iendelee hadi mwisho.

Mlalamishi huyo anataka Bw Sonko asikubaliwe kuwania kiti cha kisiasa katika uchaguzi ujao kwa msingi kuwa alibanduliwa mamlakani alipokuwa gavana wa Nairobi baada ya kupatikana na makosa ya kimaadili kinyume na Katiba.

Kesi nyingine iliyowasilishwa na mashirika matatu ya kutetea haki za umma dhidi ya Bw Sonko, inatarajiwa kutajwa leo katika Mahakama ya Mombasa.

Mashirika ya Haki Yetu, Kituo cha Sheria na Transparency International yanadai kuwa Bw Sonko hastahili kushikilia wadhifa wa kiserikali kwa kuwa alibanduliwa mamlakani kwa ukiukaji wa katiba.

Gavana huyo wa zamani anawania kurithi kiti cha Gavana Hassan Joho kupitia kwa chama cha Wiper. Chama hicho na Tume ya Uchaguzi (IEBC) pia zimetajwa kutoa majibu katika kesi hizo mbili.

Chama hicho na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) pia zimetajwa kutoa majibu katika kesi hizo mbili.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: IEBC, CA wakome malumbano ili kufanikisha...

Wazazi wapinga likizo ya katikati ya muhula

T L