Habari Mseto

Korti yasitisha agizo la kuitaka kaunti ya Nairobi ilipe mamilioni

April 22nd, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

GAVANA wa Nairobi Mike Sonko alifaulu kusitisha agizo la mahakama ambapo serikali ya kaunti ilitakiwa kulipa kampuni moja kitita cha Sh6.2milioni.

Kampuni hiyo ilikuwa imeiuzia kaunti ya Nairobi karatasi za uchapishaji.

Bw Sonko aliambia mahakama makubaliano yaliyoafikiwa kati ya kaunti na kampuni hiyo ya General Supplies hayakuwa yameidhinishwa na kamati husika katika baraza la  kaunti.

Hakimu mkuu Bi Edna Nyaloti, alisitisha utekelezaji wa agizo kwamba kampuni hiyo ilipwe pesa hizo.

Kulingana na Bw Sonko agizo hilo lilitolewa kwa njia isiyo halali.

Kesi itaendelea Aprili 25, 2018.